Habari

Kigali yaanzisha usafiri wa baiskeli kuepuka uchafuzi wa hali ya hewa

Mji wa Kigali umeanzisha aina mpya ya kusafiri mjini humo kwa kutumia baiskeli kama sehemuyajuhudi za Rwandaza kukabiliana na uchafuzi wa mazingirana kupunguza hewa ya kaboni katika miji na vituo vya miji vinavyoongezeka nchini humo.

Wasafiri wataweza kutumia baiskeli hizo za kupokezana katika mji mkuu Kigali kwa bei ya chini ikilinganishwa na usafiri mwingine uliopo mjini humo.

Kijana akienda kuchukua baiskeli kwa ajili ya kuendesha
Image caption: Kijana akienda kuchukua baiskeli kwa ajili ya kuendesha

Mjini Kigali, mtaa wa Remera baiskeli nyingi zenye rangi ya kijani na manjano zimeezekwa katika kila kona ya barabara.

Wakazi wa mji huo wanapakua application kwenye play store ya simu zao ili waweze kutumia baiskeli yetu’’ Anaeleza kijana wa kike ambaye amekuwa akitoa maelezo kwa wapita njiawanaoashuhudia jinsi ya matumizi ya maiskeli hizo.

Kuna vituo 13 vya baiskeli hizi mjini Kigali ambako pia kuna barabara maalumu za kuendeshea baiskeli. Mtaa wa Remera karibu na uwanja wa mpira kuna vituo vingina baadhi wameanza kutumia baiskeli hizi.

Barabara za baiskeli zimeandaliwa kando ya barabara kuu
Image caption: Barabara za baiskeli zimeandaliwa kando ya barabara kuu

Kwa mjibu wa kampuni ya ‘Gura Ride’ inayosimamia mpango huu anayetaka baiskeli anaichukua katika kituo kilicho karibuna kisha shughuli zake kuiweka kwenye kituo kingine kilicho karibu na mwisho wa safari yake.

Hatahivyo changamoto iliyopo bado nikwamba bado kuna barabara chache za kuendeshea baiskeli hizi mjini kigali ,pia milima iliyopo mjini Kigali inaweza kuwa kikwazo.

Barabara ziko maeneo mawili ya jiji  kwa sasa
Image caption: Barabara ziko maeneo mawili ya jiji kwa sasa

Lakini wahusika wana majibu kwa changamoto hizo, Jerry Ndayishimiye ni afisa wa GuraRide:

Meya wa jiji la Kigali Pudence Rubingisa amesema lengo kubwala mradi huuni kukabiliana na uhalibifu wa mazingira:‘’tunataka usafiri unaotusaidia kulinda uchafuzi wa mazingira, kusafiri bila kutumia magari kwani tutakaposafiri kwa kutumia baiskeli itakuwafaidakubwa kwa afya zetu kwa kupata hewa safi’’

Related Articles

Back to top button