Burudani

Kilichompeleka Nyamwela kwa Choki

Nyamwela1
(Super Nyamwelakushoto  akiwa na Beni Kinyaiya)

Mwanamuziki na dencer wa Twanga Pepeta kwa zaidi ya miaka kumi, Hassan Mussa ‘Super Nyamwela’ alikiri kwamba, muziki umekuwa kama Soccer ‘mpira’ kwa hiyo watu wategeme usajili wa mara kwa mara.Nyamwela, ambaye alikuwa kiongozi wa Madencer ‘Wanenguaji’, amesema kutoka kwake Twanga Pepeta wasimuelewe vibaya kwani yeye yupo kimasirahi kama wachezaji mpira, wakiwekewa mkwanja mezani, basi wanafanya kazi. Pia alidai sio kwamba Twanga chini ya Asha baraka ilikuwa hailimpi vizuri, la hasha ilikuwa ikimlipa vizuri ila Extra Bongo, ilizidi dau na kuamua kuhamia huko kimasirahi zaidi.

Akiongea na  Bongo5, alisema ile kauli ya maisha na muziki, imekuwa muziki ni maisha kwa hiyo hata wanamuziki inabidi waishi kwa kutumia kazi zao za kimuziki.

Amekiri kwamba bendi siku hizi, zimekuwa hazidumu kwa hiyo watu wasimuelewe vibaya kama mkataba wake utakapoisha, na kuhamia  bendi yoyote kwani anahaki ya kwenda popote, hata kama kurudi Twanga Pepeta ingawa hategemei. Anasema hapendi kuhama hama, na kama ikitokea tatizo lingine basi anaweza kusimama kama mwenyewe na kufanya kazi zake.

Miongoni mwa wanamuziki wengine waliohamia Extra Bongo , bendi inayomilikiwa na Ali Choki, kutoka bendi ya zamani ya Ali Choki Twanga Pepeta ni Danger Boy,Otilya Boniphas, na Super Nyamwela ambao ni wanenguaji, Rogart Hega ‘Katapila’ huyu ni mwimbaji, Hoseah Mgohachi na Godfrey Kanuti wakiwa kama wapiga vyombo na Saulo John ‘Farguson’ huyu ni rapper.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents