Michezo

Kilimanjaro Stars yaikosa nafasi ya 3 ya CECAFA, yafungwa na Zambia

Timu ya taifa ya Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Stars’ imeshika nafasi ya nne michuano ya Kombe la CECAFA 2013 inayofanyika nchini Kenya baada ya kufungwa na timu ya Zambia kwa penalti 6-5.

stars1

Mchezo huo uliokuwa wa kutafuta mshindi wa tatu wa kombe hilo ulikuwa na ushindani mkubwa ambapo bao la Zambia lilifungwa na Ronald Kampamba katika dakika ya 51 na Kilimanjaro Stars ilisawazisha kupitia kwa Mbwana Samatta katika dakika ya 65 kipindi cha pili ambapo dakika 90 ziliisha kwa sare ya bao 1-1.

Wachezaji wa Kilimanjaro Stars waliopata penalti ni Mbwana Samatta, Erasto Nyoni, Himid Mao, Amri Kiemba na Ramadhan Singano ‘Messi na waliokosa ni Haruna Chanongo, Mrisho Ngassa na Kelvin Yondani.

Picha hisani Bin Zubeiry

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents