Burudani

Kim Kardashian arejea kwenye mitandao ya kijamii baada ya kuisusa kwa miezi 3

Kim Kardashian amerejea tena kwenye mitandao ya kijamii Jumanne hii baada ya kuisusa kwa miezi mitatu na katika kipindi ambacho kumekuwepo na tetesi za mgogoro kwenye ndoa yake na Kanye West.

Staa huyo ambaye baada ya kuvamiwa na kuporwa mali jijini Paris, Ufaransa na kukaa kimya kwa kipindi kirefu bila kuandika chochote kwenye akaunti zake, amerejea Instagram kwa picha akiwa na mume wake, Kanye West na wanae, North, 3, na Saint, 1. Hadi sasa picha hiyo imepata comments zaidi ya 111k na likes zaidi ya milioni 3.3.

Kim pia ameupdate app yake kwa kuweka video akiwa na mume wake Kanye pamoja na watoto wao wakifurahia muda bora pamoja.

Post yake imekuja wiki kadhaa baada ya familia yake kuandamwa na matatizo ikiwemo kulazwa kwa mume wake Kanye mwezi November.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents