Bongo5 ExclusivesHabari

Kinachowaangusha wasanii chatajwa, Elimu na uongozi usiofaa

Kupitia kipindi cha RECAP & MANDO @el_mando_tz amekuja na sababu mbili kubwa zinazopelekea wasanii wetu wa Bongo Fleva kushindwa kufanya vizuri kimataifa lakini pia kuishindwa biashara ya muziki ipasavyo.

Ametaja sababu hizo kuwa ni:

  1. Kuhusu mambo Uongozi (wengi wanatumia viongozi wengi ambao ni washikaji/marafiki zao hawazingatii uweledi wa mtu husika.
  2. Eimu kwa wasanii juu ya biashara wanayoifanya ya muziki.

@el_mando_tz amemtolea mfanno Diamond kuwa ni mfano wa kuigwa kwa wasanii hapa Tanzania na hata Afrika Mashariki kutokana na anavyosimamia muziki wake na pia meneja aliowaajiri.

Mpaka sasa Diamond ana mameneja watatu kitu ambbacho ni ngumu sana wengine kumuelewa kwa haraka lakini meneja hao wote ndio wamesababisha Diamond kuwepo hapa alipo sasa.

anaongeza kuwa wasanii wengi wana ubinafsi sana juu ya kuajiri meneja ambao wanauelewa na expose juu ya muziki kwa kuwa wanaogopa kuwalipa vizuri na nndio maana wanatumia washikaji/marafiki zao ila sio watu wenye uelewa na connection kimuziki.

Amemtolea mfanno Alikiba alivyokuwa na Seven Mosha lakinni baada ya kuachana naye kuna utofauti mkubwa sana, meneja wake wa sasa sio kama hafai bali anahitaji msaidizi lakini pia kuna muda Harmonize alikuwa na Mjerumani pia kuna utofauti baada ya kuachana naye, Chopa sio kama hafai bali aongezewe mtu.

Marioo ili afanikiwe zaidi Kimataifa anatakiwa aongeze meneja mwingine ambaye atamfungulia njia Kimataifa.

Kuhusu Suala la Elimu wasanii wengi hawana uelewa juu ya streaming za nyimbo zao na platform wanazotumia kuuza muziki zinawaibia sanna kwa sababu wao uelewa hawana.

Je uankubaliana na @el_mando_tz kwa asilimia ngapi???

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents