FahamuHabari

Kipande cha kapsuli cha SpaceX chaanguka Australia kutoka angani

Wakati Mick Miners, mkulima katika eneo la New South Wales, Australia, alipoona kwa mara ya kwanza kitu kikubwa cheusi kikiwa ardhini katika sehemu ya mbali ya shamba lake, alifikiri ulikuwa mti mfu.

Lakini kwa ukaguzi wa karibu – na uhakiki kutoka kwa wataalam – aligundua kuwa kilianguka kutoka angani.

Shirika la Anga za Juu la Australia (ASA) baadaye lilisema lilitoka kwa kibonge cha SpaceX.

Wataalamu walielezea ugunduzi huo kama “nadra” na “kusisimua” – lakini walisema matukio kama hayo yanaweza kuwa ya kawaida zaidi.

Kitu hicho kilitua tarehe 9 Julai katika eneo kubwa la mashamba, lakini hakikugunduliwa na Bw Miners hadi wiki kadhaa baadaye.

Vipande vingine viwili vilipatikana baadaye, na ASA iliuliza mtu yeyote ambaye alikutana na vitu zaidi kuwasiliana nao kupitia nambari ya simu .

Dkt Brad Tucker, mwanafizikia katika Chuo Kikuu cha Kitaifa cha Australia, aliitwa kuchunguza kitu hicho.

“Hii imekuwa ya kusisimua sana kuona haya kwa karibu, sijawahi kuona kipande cha taka kikianguka hivi,” alisema kwenye video iliyowekwa mtandaoni.

Don Pollacco, profesa wa astrofizikia katika Chuo Kikuu cha Warwick cha Uingereza, alikubali kwamba ni nadra sana kwa uchafu wa anga kugonga nchi kavu.

Wakati vitu vinaanguka kutoka angani hadi Duniani kila siku, vingi hutua kwenye bahari inayofunika sehemu kubwa ya sayari, alisema.

Zaidi ya hayo, kisa pekee kilichorekodiwa cha mtu aliyepigwa ni Lottie Williams, ambaye hakujeruhiwa wakati kipande cha uchafu wa anga kilitua kwenye bega lake huko Oklahoma, Marekani, mwaka wa 1997.

Matukio mengine ni pamoja na uharibifu wa majengo nchini Ivory Coast mnamo 2020, kutoka kwa vipande vya roketi ya Uchina.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents