Habari

Kirusi cha India chatua Uganda

Sampuli kutoka kwa mtu aliyeambukizwa, ambaye anapata matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Kitaifa ya Mulago katika mji mkuu Kampala, ilichukuliwa tarehe 26 Machi.

Nchi hiyo pia imerekodi maambukizi ya aina ya virusi hivyo kutoka Uingereza, Afrika Kusini na Nigeria.

Kuthibitishwa kwa aina hiyo ya virusi kutoka India kunakuja wakati huu India inapambana na wimbi la pili la virusi ambalo limeharibu miji yake, huku hospitali zikikumbwa na uhaba wa oksijeni na vitanda na mazishi yakifanyika katika maeneo ya kuegesha magari.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Virusi nchini Uganda, Dk Pontiano Kaleebu, alisema kuwa msisitizo zaidi utalazimika kuwekwa katika hatua za kuzuia na upimaji wa watu katika mipaka ya nchi hiyo.

Uganda ilianzisha awamu ya kwanza ya kampeni yake ya chanjo mnamo Machi baada ya kupokea dozi 864,000 za chanjo ya AstraZeneca kupitia mpango wa kimataifa wa Covax, na 100,000 zaidi kutoka India.

Watu 304,000 tu wamepewa dozi ya kwanza hadi sasa.

Awamu ya kwanza inawalenga wafanyakazi walio mstari wa mbele kupambana na virusi hiyo – pamoja na wale walio katika sekta ya afya na elimu, wazee na watu wazima walio na hali nzuri ya kiafya.

Nchi ilianza kupunguza masharti makali ya kupambana na janga hilo hatua baada ya nyingine mnamo Mei mwaka jana. Hatua za kuzuia maambukizi , kama vile kuvaa barakoa na kujitenga sasa zinapuuzwa na watu wengi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents