Mke wa mchezaji wa zamani wa timu ya kikapu ya Lakers ya Marekani, Kobe Bryant, Vanessa, amejifungua mtoto wa kike na kuifanya familia hiyo kuwa na watoto watatu, wote wa kike.
Watoto wengine wa familia hiyo ni Natalia Diamante Bryant, 13, na Gianna Maria-Onore Bryant, 10. Staa huyo wa NBA na mke wake, walikutana mara ya kwanza November 1999, wakati huo Vanessa alikuwa na miaka 17 tu. Walifunga ndoa mwaka 2001.
December 2011, Vanessa aliomba talaka kutoka kwa mumewe kutokana na tetesi za mume wake kutokuwa mwaminifu, lakini waliamua kurudiana January 2013.