Burudani

Kodak Black afungwa jela mwaka mmoja

Rapa Kodak Black amehukumiwa kwenda jela kwa kipindi cha siku 364 sawa na mwaka mmoja kwa kukiuka masharti ya kifungo chake cha ndani, yaani house arrest.

Hukumu hiyo ilitolewa siku ya Alhamisi mishale ya mchana. Black, mwenye umri wa miaka 19, akiwa mbele ya mahakama alimuomba msamaha mama yake baada ya kumuona akilia nje ya mahakama

”Inaumiza moyo wangu ” ndio kauli aliyotoa rapa huyo ambaye awali alikuwa afungwe miaka nane jela kwa kosa hilo lililotokana na kwenda kujirusha kwenye bar ya strippers huko Miami bila ruhusa kutoka kwa afisa wake wa uangalizi.

Rapa Black amekuwa katika gereza la Broward huko Fort Lauderdale tangu Feb. 28 mwaka huu.

Na Laila Sued

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents