Fahamu

Fahamu: Nchi 10 Afrika zenye raia tajiri

Ifuatayo ni orodha ya Nchi zenye wananchi wenye kipato kikubwa zaidi Afrika imetolewa na Benki ya AfrAsia na New World Wealth mwezi wa 4 mwaka huu. Utajiri wao unapimwa kwa mali wanazomiliki, ikiwemo nyumba kubwa yaliopo katika Mataifa ya Ughaibuni.

1. Mauritius

Ni nchi iliyopo kwenye kisiwa, ndani ya bahari ya Hindi ikiwa na jumla ya watu milioni 1.263

2. Afrika Kusini

Inapatikana Kusini mwa bara la Afrika ikiongozwa na Rais Jacob Zuma, ina watu milioni 54.96. Lugha ya Kizulu na kiingereza ndio hutambulika zaidi.

3. Namibia

Nchi ya Namibia ipo Kusini Mashariki mwa Bara la Afrika , karibu na bahari ya Atlantic na ina jumla ya wakazi milioni 2.459

4. Bostswana

Nchi ya Bostwana inapatikana Kusini mwa bara la Afrika, na ina watu wapatao milioni 2.262

5. Egypt.Arab Republic

Inapatikana Kaskazini kati mwa Afrika,mji mkuu wao ukiwa ni Cairo.

6. Angola

Angola ni nchi inayotumia lugha ya kireno na ina watu wapatao milioni 25.02,Rais José Eduardo dos Santos ndi kiongozi wa taifa hilo

7.Algeria

Algeria ni nchi iliyopo Kaskazini mwa bara la Afrika na pia ipo karibu na bahari ya Mediterania. Nchi ya Algeria inakaribiana nchi ya Morocco.

8.Morocco

Nchi ya Morocco inakaribiana na bahari ya Altlanic, inaongozwa na Mfalme Mohamed VI. Lugha yao ikiwa ni kiarabu taifa hilo linaongozwa kwa misingi ya dini ya kiislam.

9. Kenya

Ni mora ya nchi inayopatikana katika ukanda wa Afrika Mashariki, Rais wake ni Uhuru Kenyatta. Mji mkuu wa Kenya ni Nairobi. Wakazi wa nchi hiyo hutumia lugha ya kiswhili na kiingereza katika maswasiliano.

10.Ghana
Ghana ni moja kati ya nchi zilizopo Magharibi mwa Afrika. Ina idadai ya wakazi wapatao milioni 27. 41

Raia hawa kutokea nchi hizi barani Afrika humiliki majumba kwenye miji mikubwa duniani kama New York, Paris, Geneva, London, Dubai na mengineyo.

Na Laila Sued

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents