Michezo

Koeman: Siwezi kushangaa kwa sababu hii ni mara ya tatu mfululizo napata ushindi dhidi ya Wenger

Kocha wa klabu ya Everton Ronald Koeman amemshangaa kocha Arsene Wenger kwa kulalamikia uamuzi wa refa Mark Clattenburg, baada ya Everton kupata ushindi dhidi ya Arsenal kwa mabao 2-1.

Wenger alihisi kua kuna namna ambayo ilichangia ushindi wa Everton haikuwa sahihi.

Siwezi kushangaa kwa sababu hii ni mara ya tatu mfululizo nimeshinda dhidi ya Arsenal na mara ya tatu mfululizo refa amelaumiwa alisema Koeman.

Ushindi mara mbili Koeman alipata dhidi ya Arsenal, aliupata wakati akiongozo klabu ya Southampton ambayo ilishinda kwa mabao 4-0 mwezi Desemba mwaka 2015 na kwa mabao 2-0 miezi 11 baadaye.

Kocha Wenger ameshindwa kumshinda Koeman katika mechi nne zilizopita.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents