Burudani

Kuna watu wananiroga sana – PNC

Wasanii wengi wamewahi kulalamika kuwepo kwa uchawi kwenye industry ya muziki ambayo inawapelekea kufanya vibaya, lakini waliofanikiwa wanasema ni kujituma pekee ndiyo pamewafikisha pale walipofika.

PNC 2

PNC ni miongoni mwa wasanii waliowahi kuwa chini ya menejimenti ya Tip Top Connection kabla ya kuondoka na kuelekea kwa Ostaz Juma na sasa akionekana kusimamia kazi zake binafsi.

Akiongea kwenye Stori Tatu ya Planet Bongo, inayoruka kupitia EA Radio, PNC amesema, ‘Narogwa sana ndiyo maana siweki wazi kutafuta menejimenti’.

“Bado sijapata menejimenti yangu mpya bado kazi zangu nasimamia mwenyewe. Wananiroga sana ndiyo maana sitaki kuweka wazi. Nje ya muziki ninaweza nikafanya kazi yeyote kwa sababu nimetokea kwenye maisha magumu, nimeshawahi mpaka kuchunga,” ameongeza PNC.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents