Burudani

Kwa wale wanaopenda magari ya kifahari, mrembo Kim Kardashian amekutangazia habari hii njema kwako (+picha)

Kama una ndoto ya kumiliki gari la kifahari tena sio tu la kifahari bali lililotumiwa na moja ya wanawake maarufu zaidi duniani, Mwanamitindo Kim Kardashian West basi habari hii ikufikie.

Habari ni kwamba Kim ameingiza gari lake la kifahari aina ya Land Rover Range Rover V8 2015 kwenye mnada ambapo imeripotiwa kuwa anaiuza kwa dola $85,880 sawa na tsh milioni 196.

Gari hilo tayari limeingizwa kwenye mtandao maarufu nchini Marekani wa kununua na kuuza magari yaliyotumika wa Rosso Corsa.

Mtandao huo umeandika kuwa gari hilo limetembea kilometa 35, 160 tu na gari ipo Customised kwenye kila mfumo wa uendeshaji.

Hata hivyo Kim gari hilo analiuza kwa hasara ya dola $66,000 sawa na tsh milioni 150 kutoka gharama aliyonunulia ndinga hiyo ya dola $151,000 mwaka 2015.

 

 

Related Articles

One Comment

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents