Habari

Kwanini kila mtu mwenye taaluma anatakiwa kuwa na tovuti yake binafsi

Wewe kama una weledi fulani au taaluma fulani unahitaji kujenga CV yako si ile ti unayotumia kuombea kazi bali hata kuhusu taaluma yako mwenyewe na vitu unavyofanya. Kumiliki tovuti si kwa makampuni au mashirika tu bali hata watu binafsi inasaidia watu kukupata kirahisi na kujua vitu unavyofanya.

rbrb_2557

Kutokana na ongezeko la ushindani katika ajira unahitaji kuwa mbunifu na kujua namna watu wanaweza kukufuatilia na kuona kitu unachofanya hivyo unahitaji kujitangaza sana.

Wewe kama ni mtaalamu, kuna watu wanatafuta taaluma yako na hawajui wataipataje, hivyo unapojitangaza kwenye tovuti yako na taaluma yako ni rahisi watu kujua kuwa labda, wewe ni mkandalasi wa majengo, kemikali n.k. Vile vile hiyo inapunguza mashaka ya mwajiri wako wa sasa kujua au kutojua kwamba umetuma Cv yako kampuni nyingine, kwani CV yako inapatikana na kusubiri fursa. Hebu tazama faida hizi;

1. TOVUTI YAKO INAKUSAIDIA KUPATIKA KWA URAHISI NA HARAKA ZAIDI 

Inamaanisha kuwa wakati watu wanatafuta vitu kwenye google na mitandao mingine unaweza kuonekana kwa kukusudia au kwa bahati mbaya mtu akakutana na tovuti yako. Hii inatokea wale wanaotafuta watu kwa majina hivyo jina lake linaweza kukatiza sehemu na mtu akakutambua kutokana na taaluma yako na ukatafutwa.

2. WATU WENGI SIKU HIZI KABLA YA KUKUTANA NAO WANAONEKANA KWANZA KWENYE MTANDAO

Kutokana na utafiti wa google, asilimia 80 ya watu wengi wanakutana kwenye mtandao kabla ya kukutana ana kwa ana. Na asilimia hizo huongezeka pale mwajiri anapotafuta mtu wa kuajiri, hivyo basi unapokuwa na tovuti nzuri iliyoandaliwa kwa umakini mkubwa inakujengea heshima na umaridadi wako kwa mwonekano wa kwanza kwa mtu yeyote atakayeona habari zako.

3. TOVUTI YAKO INAZIPA HABARI ZAKO UMUHIMU MKUBWA 

Vile vile watafiti wa mambo wanasema watu wengi wanatumia muda mwingi kwenye tovuti kuliko kwenye mitandao ya kijamii. hivyo bila kusumbuliwa na matangazo na watu wengine wanaoshindana kwa mwonekano wao kwenye mitandao ya kijamii mtu akikufikia utampeleka kwenye tovuti yako na kama una habari zenye maana atatumia muda mwingi hapo mpaka anachokitafuta amekipata.

4. TOVUTI INATUMA UJUMBE WENYE NGUVU KUWA WEWE NI MWENYE WELEDI

Kwa miaka migni wanasiasa, waimbaji na hata waandishi mashuhuri wametumia tovuti kuwa sehemu za kuonyesha sera na kazi zao. Unapokuwa na tovuti yako binafsi inakuonyesha unaelewa sana taaluma yako, mwonekano wako na hata habari zako. Vile vile tovuti yako inakupunguzia upotoshwaji wa habari zako, wewe ndiye unayetoa kwa mara ya kwanza hivyo ni rahisi kupambana na uzushi au uvumi wa bongo kuhusu wewe.

5. TOVUTI YAKO INAKUONGEZEA MVUTO NA INAKUFANYA UTU KWAKO  UNG’AE

Tovuti yako inakupa muda na fursa ya kuongelea vitu unavyopenda kwa namna ambayo inakuwa ngumu kuvielezea kwenye CV yako ya kawaida wakati wa kuomba kazi na inawapa watu fursa ya kuweza kuwasiliana na wewe kwa urahisi na uhakika kwakuwa wanajua mtu wanayewasiliana naye.

Awali Mwaisanila

A Personal Career Development specialist, passionate about empowering emerging generations of student, graduates and working class.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents