Michezo

Kyle Edmund atupwa nje ya michuano ya Chengdu Open

Michuano ya wazi ya Tenis nchini China ya Chengdu imeendelea tena ambapo muingereza, Kyle Edmund ameshindwa kutamba mbele ya Jared Donaldson baada ya kukubali kipigo kikali katika mchezo wa duru la pili.

Edmund ambaye alifanikiwa kumtoa, Bernard Tomic katika mchezo uliyopita amekubali kipigo cha jumla ya seti 6-0, 1-6, 6-4 kutoka kwa Jared Donaldson raia wa Marekani.

Kyle Edmund arejea kwa kishindo michuano ya Chengdu Open

Mashindano hayo ya wazi ya Chengdu ‘Chengdu Open’ inaendelea tena leo siku ya Alhamisi kwa michezo kadhaa kupigwa wakati  mchezaji, Taylor Fritz atashuka dimbani kukipiga na Nikoloz Basilashvili, Dominic Thiem  dhidi ya Guido Pella.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents