Burudani

Label ya Dully Sykes kuanza kufanya kazi rasmi Januari 2017 ‘sitaki msanii wa kunizidi’

Msanii mkongwe wa muziki Dully Sykes ameweka wazi kuwa na yeye yuko mbioni kuanzisha lebo yake ya muziki kwa lengo la kukuza vipaji vya vya muziki.

Muimbaji huyo amedai hana haja ya yeye kujiunga na lebo nyingine yoyote ya muziki kwa kuwa na yeye ana mpango huo.

“Na mimi naanzisha lebo yangu kuanzia Januari, sina haja ya kwenda kwa Diamond, nishaanza maandalizi, nina studio nina wasanii, lakini sitataka wasanii wanaonizidi, nitataka wasanii wachanga zaidi,” Dully Sykes alikiambia kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio.

Alisema kikwazo kikubwa cha wasanii wa bongo ni menejimenti kwahiyo anachotamani kufanya ni kutengeza menejimenti imara kama ilivyo kwa menejimenti za Diamond na Alikiba.

Katika hatua nyingine, muimbaji huyo ametoa taarifa rasmi kuwa anatoa ngoma mpya kabla ya mwezi Februari mwaka 2017 ambayo itakuwa ni hatari kuliko Inde.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents