Burudani

Layla (Voice Fairy) – Msanii chipukizi wa Bongo aliyeshinda shindano la Yemi Alade na kuwa staa kwa kuimba cover za wasanii

Kwa wapenzi wa mtandao wa Instagram, jina na sura ya Layla aka The Voice Fairy sio vigeni.

11253897_955031214568617_1983885996_n

Muimbaji huyo wa Mwanza anayeishi Dar es Salaam kimasomo amejipatia umaarufu kwenye ulimwengu wa Instagram kwa kuimba nyimbo za wasanii wengine (cover) kabla hata ya kurekodi wimbo wake ‘Hoi Hoi’ uliotoka wiki iliyopita.

10249313_428053124072355_1371821855_n

“Napenda sana kuimba nyimbo za watu napost kwenye Instagram yangu,” Layla alikiambia kipindi cha The Bridge cha Radio Free Africa, Jumapili, Nov 15.

“So hiyo ilinijengea nikimuimbia mtu nyimbo yake anafurahia vile. Ilinijengea umaarufu na wasanii wengi and that’s why niliweza kupata opportunity nyingi na kujuana na wasanii wengi ndani na nje ya nchi,” alisema.

12071110_1725910404305423_786737987_n

Kupitia umaarufu wake wa Instagram alishiriki pia shindano lililoandaliwa na muimbaji wa Nigeria, Yemi Alade. Zawadi ya shindano hilo aliloshinda ilikuwa ni simu ya iPhone 6 na kula dinner na Yemi Alade.

“Unfortunately mpaka leo sijapata but it’s okay,” alisema Layla.

“Naelewa [Yemi] atakuwa amekumbwa na mambo mengi na mimi sio mtu wa kung’ang’ania. Nimefurahi tu kuwa niliweza kushindana hilo shindano na nikashinda na niliweza kujifunza vitu vingi na nimeweza kujuana na watu wengi, ni promo kubwa sana kwangu.”

Anasema aliweza kufahamiana na producer wa AM Records, Manecky kupitia mdogo wake Sam aliyemfahamu Layla kupitia cover alizokuwa akizipost kwenye Instagram. Sam alimuunganisha na kaka yake Manecky aliyerekodi wimbo wake wa kwanza Hoi Hoi.

12237221_1669908713222926_427056748_n

Anadai kuwa alipanga kumshirikisha Ben Pol au Jux kwenye wimbo huo lakini haikuwa rahisi kuwapata wasanii hao katika muda aliokuwa amepanga. Usikilize wimbo huo hapo chini.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents