Diamond Platnumz na Vanessa Mdee washinda tuzo 4 za AFRIMA 2015 Nigeria

Tuzo za All Afrika Music Awards 2015 (AFRIMA) zimetolewa usiku wa Jumapili November 15 jijini Lagos, Nigeria ambapo Tanzania imetoa washindi wawili.

diamond afrima

Diamond Platnumz aliyekuwa akiwania tuzo hizo ameibuka mshindi wa vipengele 3 kikiwemo kipengele muhimu cha Msanii Bora Wa Mwaka (Artist Of The Year) ambayo ilikuwa ikiwaniwa na Alikiba, Davido, Jose Chameleone, Wizkid, Yemi Alade, Sarkodie na Flavour.

Vipengele vingine alivyoshinda Diamond ni Msanii Bora wa Kiume Afrika Mashariki (Best Male Artist in Eastern Africa) pamoja na Wimbo Bora Afrika (Nasema Nawe).

“Jus wanted to let you know that we have won the first one BEST EAST AFRICAN ARTIST OF THE YEAR! this isnfor you my fans… thanks for the Votes!!! thanks alot @the_speshoz for this Suit and many thanks to my brother @jm_international_collection for the scarf and Tie! #AfrimaAwards” alindika Diamond Instagram.

vee

Vanessa Mdee ameshinda kipengele cha ‘Best African Pop’ kupitia wimbo wake ‘Hawajui’.

Msanii mwingine wa Tanzania aliyekuwa akiwania tuzo hizo ni Linah, ambaye alikuwa akishindania kipengele cha Msanii Bora Wa Kike Afrika Mashariki hakubahatika kushinda kipengele hicho.

Related Articles

Back to top button