Michezo

Lionel Messi na Mohamed Salah vita yao bado ngumu

Mshambuliaji wa klabu ya Barcelona na Timu ya taifa ya Argentina, Lionel Messi na mshambuliaji wa Liverpool, Mohamed Salah bado wapo kwenye vita kali ya kufukuzia kiatu cha dhahabu barani Ulaya.

Tokeo la picha la messi vs mohamed salah
Mohamed Salah na Lionel Messi

Messi kwenye mchezo wa jana alishinda goli 3 kati ya magoli 4-2 waliyoshinda dhidi ya klabu ya Deportivo La Coruna.

Kwa ushindi huo Messi anafikisha idadi ya magoli (32) ya La Liga akiwa amemtangulia Mohamed Salah kwa goli moja (31).

Ingawaje Messi anamuongoza Salah lakini bado pia ana mechi nne mkononi za Ligi wakati Mohamed Salah yeye amebakiza mechi mbili za EPL.

Hata hivyo, wakati macho ya wapenzi wengi wa soka duniani wakiangalia mchuano huo wa watu wawili kwa msimu huu, bado kuna wachezaji wengine hatari zaidi ambao wanaweza wakaushangaza ulimwengu wa soka kwa msimu huu nao ni Ciro Immobile kutoka klabu ya SS Lazio na Robert Lewandowski wa Bayern Munich.

Immobile mpaka sasa ametupia magoli 29 na bado ana mechi nne mkononi huku Lewandowski akiwa na magoli 28 na mechi mbili mkononi.

Msimu uliopita 2016/17 kiatu cha dhahabu barani Ulaya kilichukuliwa na Messi ambapo alitupia magoli 37 kati ya mechi 29 alizocheza La Liga .

Kiatu cha dhahabu barani Ulaya kinatolewa kwa mchezaji mwenye magoli mengi zaidi kuliko mchezaji yoyote kwenye Ligi zote za mpira wa miguu barani humo.

Je, unadhani mwaka huu kiatu hicho kitachukuliwa nani?

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents