Michezo

Lukaku, Sanchez waibeba Man United EPL

Ligi kuu ya soka nchini Uingereza imeendelea hii leo kwa michezo kadhaa kupigwa kwenye viwanja mbali mbali huku katika dimba la Old Trafford wadau na wapenzi wa mchezo huo wakishuhudia Manchester United ikitoka na ushindi wa mabao 2 – 0 dhidi ya Swansea.

Waliyokuwa mashujaa kwenye mchezo huo ni Romelu Lukaku aliyefunga dakika ya (5) huku Alex Sanchez akifunga la pili dakika ya (20) ya kipindi cha kwanza.

Matokeo hayo sasa yanaifanya United kusalia kwenye nafasi yao ya pili kwenye msimamo wa ligi ya Uingereza kwa kuwa na jumla ya pointi 68 dhidi ya 81 ya vinara Manchester City wakati nafasi ya tatu ikishikiliwa na Liverpool wenye alama 66.

Matokeo ya michezo mingine hii leo ni Brighton 0 – 2 Leicester City, Man United 2 – 0 Swansea, Newcastle 1 – 0 Hudd’field, Watford 2 – 2 B’moith, West Brom 1 – 2 Burnley, West Ham 3 – 0 Southampton.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents