Burudani

Lulu asema hana muda wa kupoteza kwa mwanaume!

Msanii wa filamu Elizabeth Michael a.k.a Lulu amesema kuwa kwenye maisha yake kwa sasa hatakuwa na muda wa kupoteza kwenye mapenzi bali anaelekeza nguvu zake katika kazi.

Lulu-538

Akizungumza na Mwanaspoti hivi karibuni, nyota huyo wa filamu za kibongo alisema ni bora atumie muda huu kutafuta maisha ili watoto wake waje kuishi vizuri.

“Kuliko kupoteza muda na nguvu kwa mwanaume, bora nijitunze kwa ajili ya kuwalea wanangu baadaye, bado nina muda sijaishia katika Foolish Age, Mapenzi ya Mungu, bali nina kazi nyingi ninazohitaji kuzifanya ili watu wajue kwamba Lulu ana kipaji katika kazi ya sanaa na si kwamba niliingia huku kwa bahati mbaya,” alisema Lulu.

Source:Mwanaspoti

Related Articles

Leave a Reply

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents