Burudani
Lupita Nyong’o ageuka dhahabu kwenye fashion, brand kubwa zaomba kumvalisha kwenye Oscar
![](https://bongo5.com/wp-content/uploads/2014/02/lupittt.jpg)
Uigizaji wake kwenye filamu ya 12 Years A Slave umekuwa gumzo kwenye Hollywood – na sasa Lupita Nyong’o ni dhahabu kwenye ulimwengu wa fashion pia.
Brand kubwa za Uingereza zikiwemo za Stella McCartney na Alexander McQueen, zinamuomba staa huyo wa Kenya kuvaa magauni yake kwenye tuzo za Oscar. Lupita ambaye ametajwa kuwania tuzo ya muigizaji bora msaidizi wa kike kwenye Oscar, alivaa nguo ya Dior kwenye red carpet ya tuzo za BAFTA.