Burudani

Luteni Kalama adai Gangwe Mob itarudi ikipata management

Member wa kundi la Gangwe Mob, Luteni Kalama amesema kitu kinacholikwamisha kundi hilo ni management na kwamba kama ikipatikana litarejea tena.

gangwe-mobb

Luteni amesema kama wakipata management kundi hilo linaloundwa na yeye na Inspekta Haroun litasimama vizuri.

“Gangwe Mob kama Gangwe Mob itaendelea kuwepo sema kwa sasa hivi kila mtu anafanya project zake binafsi,” Kalama alikiambia kipindi cha XXL cha Clouds FM jana.

“Ujue Gangwe Mob ni crew tunategemea labda tukipata meneja hivi ambaye anaweza kusimamia project kwa sababu sasa hivi kiukweli hatuwezi kufanya wenyewe kwa sababu hatuna management ya pamoja. Inspekta yeye ana mambo yake na mimi na mambo yangu.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents