Burudani

Ray C aomba msamaha baada ya video yake akiwa mtupu kupostiwa kwenye akaunti yake ya Instagram

Siku ya jana Nov.10 kuna video mbaya ya mwanadada Rehema Chalamila maarufu kama Ray C akiwa mtupu akikata mauno zilipostiwa kwenye akaunti yake ya Instagram (@rayc1982) na muda mfupi baadaye kufutwa.

Ray new

Akizungumza na U Heard ya Clouds Fm leo, Ray C amekiri kuwa ni kweli aliyeonekana kwenye video hiyo ni yeye.

“Ndio ni kweli video hiyo ilipostiwa kwenye akaunti yangu ila sio mimi niliyeipost.” Alisema Ray C.

Ray C aliongeza kuwa video hiyo alirekodiwa na mpenzi wake kwaajili ya matumizi binafsi, lakini kwa bahati mbaya aliibiwa simu, na mtu aliyeipost anamfahamu kwasababu ni rafiki yake.

“Niliibiwa Simu yangu ilikua juzi na kuna mtu ni rafiki yangu ninamfahamu akaingia kwenye gallery nakuzipost… si log out sababu kama unavyojua ni simu yangu. Ni mpenzi wangu aliyenirekodi ile video na ilikua private Kwa ajili yetu tu.. ila kwa sasa nimeshatoa taarifa Vodacom na wamei-block ile line pia ile video niliifuta”.

Ray C alimaliza kwa kuomba msamaha kwa mashabiki wake na watu wote kwa ujumla;

“Niombe tu msamaha maana sijui hata naanzaje kuelezea… naomba tu waelewe kwamba simu nimeibiwa na mtu ambaye amefanya hivyo namjua na nimeripoti Polisi.. naomba tu msamaha.” alimaliza Ray C

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents