Michezo

Mabao ya Neymar, Cavani yamuachisha kazi Ancelotti

Uongozi wa klabu ya Bayern Munich umeamua kumfungashia virago kocha wao, Carlo Ancelotti mara baada ya kukubali kipigo cha mabao 3-0 kutoka kwa Paris Saint-Germain katika michuano ya Klabu bingwa barani Ulaya.

Maamuzi hayo yamekuja baada ya uongozi wa timu hiyo kufanya kikao mchana wa leo na kutangaza kumuachisha kazi meneja huyo mwenye umri wa miaka 58 ambapo ameachana na Bavarians rasmi.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka katika tovuti ya klabu hiyo inasema kuwa

“Kufuatia uchambuzi wa kina uliyofanywa leo siku ya Alhamisi ya Septemba 28 mwaka 2017, klabu ya FC Bayern München imeadhimia kutangaza kuachana na kocha wake Carlo Ancelotti na mwalimu msaidizi, Willy Sagnol atakaimu nafasi yake kwa muda”.

Ancelotti ambaye aliwahi kuwa kocha wa klabu ya Chelsea na AC Milan alianza kuitumikia kikosi hicho cha Allianz Arena kwa takribani miezi 15 akichukua mikoba iliyoachwa wazi na Pep Guardiola Juli mwaka 2016.

Ancelotti ameiongoza Bayern katika ligi kuu ya Bundesliga na kufanya vyema huku akishiriki michuano ya klabu bingwa barani ulaya kwa mara ya kwanza mwaka jana na kutolewa na Real Madrid katika hatua ya robo fainali  baada ya kupigwa jumla ya mabao 3-2 na kisha kufungwa na Borussia Dortmund katika hatua ya nusu fainali ya michuano ya DFB-Pokal Cup.

Meneja huyo raia wa Italia alianza kwa presha katika hatua za awali baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-0 dhidi ya Hoffenheim mwezi Septemba kisha kufuatiwa na sare ya mabao 2-2 wakiwa nyumbani dhidi ya Wolfsburg kabla ya kuja kukubali kipigo cha mabao 3-0 kutoka kwa PSG mchezo uliyochezwa jana usiku jijini Paris.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents