Burudani

Madee adai Dogo Janja amefanikiwa asilimia 92 katika uvaaji

Msanii Madee amesema msanii mwenzake, Dogo Janja, ambaye yupo chini ya Tip Top Connection, amefanikiwa katika uvaaji kwa asilimia 92 kitu ambacho walikaa nae chini na kumshauri.

Madee

Madee amekiambia kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio kuwa kitu ambacho sasa hivi mwanamuziki yeyote anatakiwa kikiweka mbele ni muonekano ukiacha kipaji.

“Sisi ambao tumeanza zamani, hivi vitu tulikuwa tunavichukulia kawaida tu lakini sasa hivi ili mwanamuziki uonekane mzuri ni muuonekano kwanza kwenye mwili na mavazi.

“Hicho ndio kitu tulijaribu kumshauri Janja na tukakaa naye vizuri na kumueleza na ndio kitu amefanya na amefanikiwa kwa asimilimia 92 na baada ya siku kadhaa naamini tutafika kule ambapo tunataka Janja awe na ule muuonekano,” amsema Madee.

Dogo Janja

Kuhusu wimbo mpya wa Dogo Janja ‘Ukivaaje Unapendeza’, Madee amesema huo ni wimbo wa ujana zaidi na kisasa kwa sababu sasa hivi kuna vijana wengi wanajitahidi kwenye kuvaa na kuonekana.

“Janja anazungumzia tu mavazi anawauliza marafiki zake, mashabiki, watu wake wa karibu wakivaa nguo gani wanakuwa comfortable kwenda sehemu yeyote. Kwa hiyo yeye anaelezea kuwa akivaa boxer, pensi, sing land, kanzu, suruali anajihisi yuko comfortable anapendeza, kwa hiyo anakuachia swali wewe rafiki yake unavaaje unapendeza?,” amemaliza kwa kusema Madee.

By Peter Akaro

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents