Habari

Magereza zatakiwa kutumia rasilimali walizonazo vizuri

Mkuu wa Magereza nchini, Kamishina Jenerali Juma Malewa ametoa wito kwa askari wa jeshi hilo kutumia kikamilifu rasilimali zilizopo ndani ya vituo vyao kutengeneza vifaa vitakavyo tumika kujenga nyumba za makazi ya jeshi hilo kwa bei nafuu.

Kamishna Jenerali Malewa ameyasema hayo mkoa Pwani baada ya kufanya ziara ya kutembelea mkoa huo kukagua miundombinu katika gereza la maabusu la Mkuza,picha ya ndege, gereza la Kigongili wilayani Bagamoyo na kuweka jiwe la msingi katika gereza la Mkuza.

“Pamoja na changamoto nyingi ambazo nimezikuta changamoto kubwa ni makazi ya askari nyumba za askari hazitoshi zilizokuwepo zimechakaa zingine zinahitaji ukarabati mkubwa tu, nimekuja kujionea mwenyewe hali halisi ilivyo ili nikirudi ofisini nione tunafanyaje ili tuweze kusaidia angalau kukarabati ili ziwe katika hali nzuri,lakini kubwa tunalolitaka kwa askari wetu nikutumia rasilimali zilizopo katika vituo vyao vizuri,” alisema Kamishna Jenerali Malewa.

Pia Kamishna Jenerali Malewa alikutana na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evaristi Ndikilo ambapo mbali na kuzungumzia makazi duni ya askari, Mkuu wa mkoa huyo amemuomba Jenerali Malewa kuangalia namna ya uboresha wa maslahi kwa watumishi wake.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents