Habari

Mahakama yatupa maombi ya wabunge 8 waliotimuliwa CUF (+Picha)

Mahakama Kuu ya Tanzania, imeyatupilia mbali maombi ya waliokuwa wabunge wa viti maalum wa Chama cha Wananchi (CUF), waliokuwa wakipinga kuapishwa kwa wabunge walioteuliwa wa Chama hicho.

Walifungua maombi hayo Mahakamani hapo wakiiomba Mahakama itoe amri ya zuio kwa Bunge lisiwaapishe wabunge hao walioteuliwa hadi pale kesi yao ya msingi kupinga kufutwa Uanachama wa chama hicho itakapotolewa hukumu.

Mahakama Kuu imeyatupilia mbali maombi hayo, baada ya kukubaliana na hoja za mapingamizi zilizowasilishwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) kupitia mawakili nane wa serikali wakiongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu, Gabriel Malata, na wakili wa Bodi ya Wadhamini CUF pamoja na wabunge wateule.

Akizungumza na wanahabari, Wakili wa CUF, Mashaka Ngole amesema kuwa pingamizi hilo linatokana na sababu za Jaji Lugano Mwandamo kusema kifungu kilichotumiwa na wabunge hao kuweka zuio sio sahihi . Hivyo basi wabunge teule ambao wako 8 wanaweza kuapishwa muda wowote.

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents