Michezo

EUFA Play-Off Draw: Liverpool wapangwa na wababe wa Bayern Munich

Droo ya mechi za kuwania kuingia kwenye makundi ya klabu bingwa barani Ulaya tayari imetolewa na Shirikisho la soka barani humo (EUFA) ambapo klabu ya Liverpool kutoka Uingereza imepangwa na klabu ya 1899 Hoffenheim ya Ujerumani.

Ratiba kamili

Kwenye droo hiyo mechi nyingine ambazo zitakuwa na msisimko ni Napoli dhidi ya Nice kutoka nchini Ufaransa na mechi kati ya Celtic dhidi ya Astana.

Liverpool wataanzia ugenini huko Ujerumani tarehe 15 Agosti na kumalizia ratiba yao pale Anfield tarehe 22 Agosti dhidi ya Hoffenheim, klabu iliyoonesha upinzani mkubwa msimu uliyopita dhidi ya mabingwa wa Bundesliga, Bayern Munich kwa kuchukua pointi 4 ya mechi za Ligi.

Kwenye droo hiyo yenye timu 20 mechi zitaanza kuchezwa kuanzia Tarehe 15/16 Agosti na mechi za marudiano zitachezwa kati ya tarehe 22/23 Agosti mwaka huu.

By Godfrey Mgallah

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents