Burudani

Majambazi wavamia na kupora nyumbani kwa rapper Big Sean

Nyumba ya rapper Big Sean wa Marekani ilivamiwa na majambazi wakati akiwa nje ya nchi.

big-sean

Kwa mujibu wa TMZ, wezi hao walivunja nyumba yake iliyopo jijini Los Angeles na kuvunja sehemu palipokuwa pamehifadhiwa vitu vya thamani. Walipora vidani vya madini vyenye thamani ya $150,000 pamoja na nyimbo ambazo bado hazijatoka.

Sean na wenzake wanaamini kuwa wizi huo umefanywa na watu wa karibu. Wezi hao walijua kuwa rapper huyo hakuwepo na walikuwa wanaijua vyema nyumba yake. Hadi sasa hakuna washukiwa wowote.

Rapper huyo alikuwa kwenye show mjini Dubai.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents