Burudani

#TECNOOwntheStage: Banye wa Tanzania aondolewa

Episode ya nne ya shindano la kusaka vipaji vya kuimba kwa mfumo wa karaoke linalohusisha nchi tatu, TECNO Own the Stage imeruka jana Jumapili kupitia Africa Magic Showcase.

Banye
Washiriki walipokuwa wakisubiri kujua hatma yao

Episode hiyo ilijumuisha washiriki wa kundi la 3 waliotakiwa kuimba nyimbo za kiafrika. Ikiwa na ushindani mkali, washiriki wa Tanzania waliopanda jukwaani ni pamoja na Banye, Mary, Jeff Mduma na Zooccu.
Hata hivyo Tanzania imepata pigo baada ya mshiriki wake Banye kuondolewa.

DSC_2486-2
Banye

Banye aliyejaribu kutafuta tobo kupitia hit ya Diamond Platnumz, ‘Number One’ alijikuta akishindwa kumshawishi jaji Bien wa kundi la Sauti Sol.

DSC_2412-2
Majaji: Bien, Yemi Alade na M.I

Alisema alishindwa kucheza vizuri na sauti yake huku Yemi Alade akishindwa kumwelewa kwanini alivaa nguo za kiafrika na chini akiwa na kiatu cha Nike!

Mary ndiye aliyekuwa wa kwanza kutupa karata yake kwa kuimba wimbo wa msanii wa Afrika Kusini, Zahara uitwao Loliwe. Mary alimkuna jaji, Yemi Alade aliyependa mashairi na kukiri kuwa licha ya kutoelewa maana yake alifurahi tu show yake.

DSC_2442-2
Mary

Zooccu aliamua kutupa karata yake kwa kuimba wimbo wa Jux, ‘Sisikii na kupata tiki kutoka kwa Yemi alipenda kile alichokisikia.
Jeff Mduma alimpa shavu Jaguar wa Kenya kwa wimbo wake Kioo na kuwavutia watazamaji waliommwagia mvua ya makofi.

Bien alifurahi kuwa Jeff alirudi kwa kasi ukilinganisha na show yake iliyopita huku M.I. akimsifia kwa kupambana kumiliki jukwaa. Yemi pia alipenda performance yake.

DSC_2553-2

Washiriki walioponea chupu chupu jana ni Tosin wa Nigeria ma Mary wa Tanzania.

Usipitwe na show hiyo kila siku za Jumapili kupitia Africa Magic Showcase saa tatu usiku na Maisha Magic East na Bongo kuanzia saa mbili na nusu usiku.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents