Michezo

Malinzi: Kila la kheri Serengeti Boys

Zikiwa zimesalia siku mbili kwa Serengeti Boys kuwasili katika kituo chao cha mashindano, Rais wa shirikisho la mpira wa miguu nchini, TFF, Jamal Emil Malinzi awatakia mafanikio barobaro hao wa Tanzania, Vijana wa Serengeti Boys katika safari yao ya kuelekea Gabon wakitokea Cameroon walipokuwa na kambi ya muda mfupi.

“Nitoe fursa hii Kuwatakia kila lakheri vijana wetu, wasafiri salama, wafike salama Libreville wafanye mazoezi. Kikosi kilichofika Libreville kina watu 34, mwanzoni tulitakiwa tuwe na vijana 21 ambao wamesajiliwa kwa ajili ya mashindano  lakini CAF wamekaa wameamua kuongeza mtu mmoja, kwa hiyo kila timu itakuwa imesajili watu 22”.

“Na niseme tu kwa kifupi  kwamba Advance partY ya Tff ipo Gabon tayari, kwa ajili ya kuhakikisha inakagua kile ambacho tutapika, inakagua viwanja ,inakagua viwanja vya mazoezi, inakagua mabasi ambayo tutatumia, inakagua Jikoni pale kwenye hoteli kuhakikisha chakula ambacho kitaendana na jinsi makocha wetu wanavyopenda”.

“kwa hiyo kikosi cha utangulizi kipo pale na mechi yetu ya kwanza  itafanyika tarehe 15 saa 9 za mchana za Gabon ambayo itakua ni majira ya saa 12 jioni kwa Tanzania. Tunaanza na Mali na tarehe 18 saa 9 mchana pia tutacheza na Niger mechi ya pili na mechi ya tatu hatua ya makundi itafanyika Jumapili tarehe 21 tutacheza usiku na Angola”.

BY HAMZA FUMO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents