Habari

Mama aliyechomwa visu 25 Moshi afariki dunia, wananchi walia mtuhumiwa yupo mtaani

Beatrice Minja (45) mkazi wa kijiji cha Mbomai juu kata ya Tarakea mkoani Kilimanjaro amefariki dunia baada ya kuchomwa kwa kisu mara 25 mwili mwake na kukaa ICU kwa siku 46 katika hospitali ya Kcmc.

Beatrice Minja alishambuliwa siku ya tarehe 12/11/2023 katika kijiji hicho majira ya jioni alipokua akitokea katika majukumu yake na mtu ambaye mpka sasa hajakamatwa na jeshi la polisi.

Akizungumzia tukio hilo mtoto wa marehemu, amesema mama yake alikua akifuatiliwa na kupewa vitisho na mtu ambaye hawakumtaja jina na aliripoti kituo cha polisi lakini aliachiwa kwa dhamana na aliendelea na vitisho na baadae mama yake kujeruhiwa.

Aidha mama mzazi wa marehemu ambaye hata hivyo naye ni mgonjwa amesema mwanaye (Marehemu) ndiye alikua tegemezi lake kwani hajiwezi na muda wote ni wa kunyanyuliwa na kuiomba serikali kumtia nguvuni aliyehusika na tukio hilo.

Jeshi la polisi Nchini limetoa taarifa mchana huu likielezea kuwa hatua za haraka za uchunguzi zitaanza ili kubaini ukweli wa jambo hilo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents