Mambo ya Richmond yaiva

KAMATI teule ya Bunge iliyochunguza mkataba wa zabuni ya jenereta za umeme wa dharura ya kampuni ya Richmond Development Limited, imekabidhi ripoti yake.

Na Gladness Mboma



KAMATI teule ya Bunge iliyochunguza mkataba wa zabuni ya jenereta za umeme wa dharura ya kampuni ya Richmond Development Limited, imekabidhi ripoti yake.


Hata hivyo kinyume na ilivyokuwa imetarajiwa, kampuni hiyo kumkabidhi Spika wa Bunge, Bw. Samwel Sitta, ripoti hiyo ilikabidhiwa kwa Ofisi ya Spika kutokana na yeye kuwa safarini nje ya nchi.


Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Dkt. Harrison Mwakyembe, alisema Dar es Salaam jana kuwa ripoti hiyo waliikabidhi jana ofisini kwa Spika ambaye yuko safarini nje ya nchi.


Dkt. Mwakyembe alisema Spika mwenyewe ndiye atakayepanga ni siku gani ataonana na waandishi wa habari ili aweze kuwapa ufafanuzi kuhusu yaliyo ndani ya ripoti hiyo.


“Spika alipenda sana awepo wakati tunakabidhi ripoti hii, lakini yuko nje ya nchi na sisi hatuwezi kuzunguka nayo katika majimbo yetu kwa sababu hii ni siri nyeti,” alisema Dkt. Mwakyembe.


Alisema kuwa kwa sasa wanaelekea katika majimbo yao kwa kuwa ni muda mrefu hawajaonana na wapiga kura wao na ndio maana wakalazimika kuikabidhi ripoti hiyo ofisini kwa spika ili ihifadhiwe.



Kamati hiyo awali ilipangiwa kukabidhi ripoti hiyo Desemba 15 mwaka jana, lakini haikiufanya hivyo kutokaba na kutokamilika kwake na hivyo kuomba kuongezwa muda.


Sababu kuu mbili zilizofanya Kamati kuongezwa muda ni kutokana na mkanganyikoi wa uahshidi lakini pia na baadhi ya wajumbe wake kulazimika kwenda Marekani kufanya uchunguzi zaidi.


Kamati hiyo ya Bunge iliundwa rasmi Novemba 13 mwaka huu na kuanza kazi siku mbili baadaye ikiwa na hadidu za rejea za kuchunguza na kubaini kampuni ya Richmond ni ya akina nani na inafanya kazi zipi.


Pia ilitakiwa kufanya tathmini ya mchakato wautoaji zabuni kwa kampuni hiyo na mkataba kati yake na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na kuangalia pia taarifa ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) na mambo mebngine kadhaa.


Wajumbe wengine wa Kamati hiyo ni Mbunge wa Muheza, Bw. Herbert Mntangi, Mbunge wa Viti Maalumu, Bibi Stella Manyanya, Mbunge wa Mkanyageni, Bw. Mohamed Mnyaa na Mbunge wa Nzega, Bw. Lucas Selelii.


Source: Majira

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents