Habari

Man Dojo na Domo Kaya wako fresh zaidi ya kawaida lakini hawana haraka..

Ukikutana na Man Dojo na Domo Kaya na ukae nao kwa dakika chache tu, utaondoka mbavu zikiwa zinauma. Wana vituko, wanaonekana wameridhika na hawana haraka kabisa ya kuachia wimbo mpya hivi karibuni.

page

Nilibahatika kukutana nao wakati wa shooting ya video ya Kama Zamani ya Mwana FA January mwaka huu na kupiga nao story. Walisema wapo kimya lakini maisha yanaendelea vizuri huku wakiwa na miradi yao binafsi inayowazesha waendelee kuzitunza familia zao bila wasiwasi.

DOJO DUKANI1
Life Goes On: Man Dojo akiwa kwenye duka lao la viatu maeneo ya Kariakoo jijini Dar es Salaam

Man Dojo anasema uhusiano wake na Domo Kaya umetoka kwenye urafiki na sasa wanachukuliana kama ndugu kutokana na kuwa na historia ndefu pamoja.

“Muziki kwa sasa hivi sisi bado tunauangalia, hatujajua inakuwaje hapo mbele mbele ila wataelewa sisi tukishaingia mzigoni kama kawaida,” alisema Domo Kaya.

Kwa sasa wasanii hao waliohit na ngoma kama Nikupe Nini, Wanoknok, Dingi na Taswira hivi karibuni walisikika tena kwenye wimbo walioshirikishwa na Mwana FA, Kama Zamani.

http://www.youtube.com/watch?v=I01yby6VmTg

Namna ambavyo wanapendwa, ilidhihirika siku ya show ya Mwana FA ya The Finest iliyofanyika June 14 jijini Dar es Salaam. Wasanii hao walimsindikiza Mwana FA kuanzia mwanzo hadi mwisho wa show hiyo ambapo licha ya kuimba back vocals na bendi, waliperform pia wimbo wao, Nikupe Nini. Wakiwa wameubadilisha na kuuongezea utamu zaidi, waliuamsha ukumbi mzima wa Makumbusho ya Taifa na shangwe kubwa kusikika wakati wakiimba.

Pamoja na kuwa kimya, kwa sasa wasanii hao wanaonesha kuiva haswaa kwenye muziki wa live jambo lililomfanya Sandu Mpanda aka Kidboy ambaye ni producer pia kusema kuwa wasanii hawa walitakiwa kuwa na bendi yao inayopiga sehemu na ambayo ingewapa fedha nyingi.

Ukimya wao umetengeneza demand kubwa ya nyimbo zao mpya na hivyo thamani yao kuendelea kuwa juu. Kama wakirejea tena hasa, Man Dojo na Domo Kaya bado wana nafasi kubwa ya kuhit nchini.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents