Michezo

Manara amcharukia Dismas Ten ”huna hamasa na hutoi taarifa kiweledi njoo nikupe elimu hii”

Mara baada ya klabu ya Simba kufanikiwa kuchomoza na ushindi mwembamba wa bao 1 – 0 dhidi ya hasimu wake Yanga afisa habari wa timu hiyo, Haji Manara amemjibu mpinzani wake, Dismas Ten kwakumuambia amekosa hamasa na weledi na hivyo anapaswa kwenda kusoma kutoka kwake.

Ujasiri huo wa Haji Manara unakuja kwenye kipindi hiki ambacho klabu yake ya Simba ikiwa mbele kwenye msimamo wa ligi kuu kwa jumla ya pointi 62 mbali kabisa nyuma ya anaemfuatia Yanga wenye alama 48 huku wakihitaji pointi nne pekee kutangaza Ubingwa msimu huu wa 2017/18.

 

hajismanaraNilikuwekea akiba..nikasema ipo siku ntakujibu…

Haji Manara amcharukia Dismas Ten ”huna hamasa na hutoi taarifa kiweledi njoo nikupe elimu hii”
Bro ww bado sana..unatumia lugha za mafumbo ambazo haziisaidii klabu.. huna hamasa na hutoi taarifa kiweledi na kwa matakwa ya sasa ya soka na soko..njoo nikupe elimu hii..jtatu iliopita ulisema Yanga lazma watashinda..haya kiko wapi?leo nimeweka picha yako na nakutag ili walau watu wakujue kdogo….
Hii ndio Simba bro…okey karibu town @dismasten

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents