Burudani

Haji Manara ashindwa kujizuia, Aingilia kati sakata la Diamond na Mhe. Shonza

Baada ya msanii wa muziki nchini Tanzania, Diamond Platnumz kutamka wazi kuwa Serikali kupitia wizara yake ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kushirikiana BASATA hawajamfanyia haki kwa kufungia nyimbo zake, Hatimaye Msemaji wa Klabu ya Simba, Haji Manara ameingilia kati suala hilo kwa kutoa ushauri .

Tokeo la picha la haji manara
Haji Manara

Haji Manara amesema kuwa Diamond kama binadamu mwingine anaweza kukosea lakini ni vyema Serikali kushirikiana na BASATA wakatambua kuwa muziki wetu umekua na unahitaji vitu gani kabla ya kufungia kazi za msanii.

Inawezekana labda (Diamond Platnumz) kama binadaamu anaweza kuwa kakosea ila tutambue muziki wa kisasa na mahitaji ya soko yanataka nini by the way Diamond na wenzie tunawatumia sana kwa mambo ya kijamii na hata kampeni zetu za kisiasa na huyu ni brand kubwa,“ameeleza Haji Manara kwenye ukurasa wake wa Instagram na kutoa ushauri.

Angalau tufanye staha kidogo na tupende vya kwetu, mimi napenda muziki mzuri sina cha timu wala baba yake timu,“amemaliza Haji Manara.

Siku ya Jumatatu Machi 19, 2018 Diamond Platnumz akiwa kwenye mahojiano na kituo cha Times FM alinukuliwa akisema kuwa viongozi wenye mamlaka serikalini wamekuwa wakifungia kazi za wasanii bila kujua gharama na muda wanaopoteza kwenye kuandaa kazi zao, huku akimlenga Naibu Waziri wa Habari, Juliana Shonza.

Hata hivyo, Mhe. Shonza akijibu tuhuma hizo kwenye mahojiano yake na Mwananchi Digital alisema kuwa hawezi kumjibu Diamond kwani alitakiwa kuwasilisha malalamiko yake kwa njia ya barua.

Mwanzoni mwa mwezi Machi, BASATA kushirikiana na TCRA ilitangaza kufungia nyimbo 15 ambapo kwenye nyimbo hizo Diamond Platnumz alifungiwa nyimbo mbili.

Baadaye Naibu Waziri wa Habari, Mhe. Juliana Shonza alitoa tamko la kumfungia rapa Roma Mkatoliki kifungo cha miezi sita kutojihusisha na muziki wala nyimbo zake kupigwa kwenye radio/Tv .

SOMA ZAIDI – Roma Mkatoliki apigwa ‘STOP’ kufanya muziki, Nay wa Mitego apewa onyo kali 

Mbali na adhabu hiyo ya kufungia nyimbo, Mhe. Shonza aliibua tena hoja nyingine iliyoleta mijadala mizito kwa wasanii na wadau wa muziki, baada ya kutamka kuwa nyimbo zote zilizofungiwa na serikali hazitaruhusiwa kutumiwa na wasanii husika hata kwenye show za nje ya nchi.

Soma zaidi – Naibu Waziri Shonza  adai sheria hairuhusu wimbo uliofungiwa msanii kuufanyia show nje ya nchi 

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents