Michezo
Manchester United nje kombe la Capital One
Mechi za kombe la Capital One ziliendelea tena October 28 usiku.
Miongoni mwa mechi zilizochezwa ni pamoja na Manchester City dhidi ya Crystal Palace. Mchezo huo ulichezwa katika dimba la Etihad. Man City wakiwa katika uwanja wao wa nyumbani wamefanikiwa kuibuka na ushindi mnono wa jumla ya magoli 5-1.
Manchester United 0 – 0 Middlesbrough ( mikwaju ya penati Manchester United 1-3 Middlesbrough). Liverpool 1 – 0 AFC Bournemouth. Huu ulikuwa ni ushindi wa kwanza kwa kocha Jurgen Klopp.
Nayo Southampton ilishinda mabao 2 – 1 dhidi ya Aston Villa.