Burudani

Mapacha wang’oa mwingine Twanga

 

Mapacha
Mnenguaji, Sabri Pozi, aliyekuwa anapiga kazi na bendi ya African Stars Twanga Pepeta amehamia rasmi kwa Mapacha watatu.


Akizungumzia uhamisho huo, msemaji wa Mapacha watatu, Dakota alisema mnenguaji huyo amehamia kwa mapacha watatu baada ya kufikia makubaliano, ambayo mnenguaji huyo alitaka yatimizwe.

Akijibu swali la kwamba haoni kuwa kitendo cha kumchukua mnenguaji huyo kitaleta bifu kati yake Dakota ama Mapacha watatu na bendi ya Twanga, Dakota alisema haoni sababu kwani suala hilo ni la kawaida kwenye ushindani wa biashara hususan ya kimuziki.

Naye Mnenguaji Sabrina ambaye anajulikana zaidi kama Loketo Mbete Mbete amesema amerudi bongo leo toka Dubai ambako alikuwa kwenye shughuli za kikazi na hivyo alikuwa akiwasiliana na Mapacha watatu kwa simu na hakusita kuchukua uamuzi wa kuhama baada ya uongozi wa mapacha watatu kumpa ofa na yeye kuwapa masharti ambayo wameyatimiza hivyo amefurahi kuhamia kwa wasanii hao kupiga kazi.

Sabrina aliendelea kusema haoni kuhama kwake Twanga ni tatizo kwani amewataarifu na kupata baraka za uongozi wa bendi ya Twanga na anafikiri hilo sio jambo geni kwake kwani alishafanya hivyo huko nyuma kwa kuhama toka Fm Academia na kwenda Twanga na sasa kuhamia kwa Mapacha watatu.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents