Habari

Mara kumi uvunje sheria uokoe fedha za Watanzania -Rais Magufuli

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Dkt John Pombe Magufuli, ameviasa vyombo vya usalama kutimiza wajibu wao kwa kusimamia rasilimali za taifa ambazo zinatumiwa ovyo na watu waliotanguliza maslahi yao mbele kwa kuviagiza kuwashughulikia ili kuokoa fedha za Watanzania.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Dkt John Pombe Magufuli

Akizungumza Ikulu leo, jijini Dar es salaam baada ya kukabidhiwa ripoti ya Almasi na Tanzanite na Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa, Rais Magufuli amesema ni bora hata sheria isifuatwe lakini uokoe fedha za Watanzania.

Niviombe Vyombo vya Ulinzi na usalama, simamieni rasilimali za Watanzania, Msisite kumshughulikia mtu yoyote anayechezea mali za Watanzamia, mara kumi uvunje sheria lakini ukiwa umeokoa fedha za mtanzania, mjipange na mnaweza kuleta strategy namna gani sasa mnaweza kulinda Tanzanite, Mkiamua mtaweza wote, mkikaa pamoja mkaamua sasa tunalinda Tanzanite, hakuna mtu atakuja kuchezea pale… Hakuna ubaya pale kulinda na SMG ni mali yetu, kila anayepita anayeenda kuchimba mle anasachekiwa analipa percentage yetu inakuwa rekodedi unampeleka anenda kuuza ndiyo utaratibu unaotakiwa.“amesema Rais Magufuli.

Hata hivyo, Rais Magufuli ameendelea kusisitiza kuwa Watanzania tujenge uzalendo na kuilinda nchi yetu ili tuweze kusonga mbele.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents