BurudaniFahamuHabari

Marapa Marekani wanaotoza kiasi kikubwa kuwashirikisha

Majarida mbalimbali nchini Marekani yameorodhesha rapper 10 ambao wanachaji kiasi kikubwa sana cha pesa kwa ajili ya kumshirikisha kwenye wimbo wako wowote ule.

Katika orodha hiyo mkongwe Marshall Bruce Mathers III alimaarufu kama Eminem kwenye umri wa miaka 50 amewafunika vijana wengi sana kwenye suala la kuchaji kiasi cha pesa ili umshirikishe kwenye wimbo wako.

Eminem anachaji dola milioni 3 sawa na Tsh 7,020,000,000/=  yaani bilioni saba huku akifuatiwa na Drake ambaye anachaji kiasi cha dola milioni 1 ambazo ni sawa Tsh 2340000000/= yaani bilioni 2.34.

Wakongwe wawili Jay Z pamoja na Kanye West imeelezwa kuwa wao wanachozingatia ni heshima na msanii husika pia mahusianno lakini kikubwa zaidi wanazingatia kile ulichoimba kwa maana kwamba ubora wa wimbo wako.

Jay Z kweye mahojianno yake na Kevin Heart kwenye ‘Hart to Heart’ ajibu swali hilo na kusema yeye hatozi hata senti moja kwa msanii yoyote akitaka kumshirikisha bali annachjozingatia ni heshima na msanii husika lakini pia aina ya wimbo anaoshirikishwa.

Katika orodha hiyo rapper ambaye wengi hawakutarajia ni J Cole ambaye anachaji dola 2,000 sawa na Tsh 4,680,000/= yaani milioni nne na laki sita za Kitanzania.

Katika orodha hiyo wengi wame-comment wakishauri Future anatakiuwa kuongeza malipo yake huku wakisema kuwa dola laki mbili na nusu ambazo ni sawa nna T sh 585,000,000/= yaani zaidi ya milioni mia tano sio saizi yake.

 

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents