Habari

Marekani yaionya China dhidi ya Taiwan

Marekani imeionya China kuhusu shinikizo zake dhidi ya Taiwan. Wizara ya mambo ya nje ya Marekani imesema hayo jana wakati ambapo mataifa hayo mawili yanajiandaa kwa mkutano wa kilele uliosubiriwa kwa hamu.

US warns China over pressure on Taiwan

Katika taarifa, wizara hiyo imesema kuwa waziri wake Antony Blinken, alizungumza na mwenzake wa China Wang Yi na kuelezea wasiwasi kuhusu ongezeko la shinikizo za kijeshi, kidiplomasia na kiuchumi dhidi ya Taiwan.

Blinken na Wang walizungumza siku ya Ijumaa ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mkutano kati ya Rais wa Marekani Joe Biden na mwenzake wa China Xi Jinping unaotarajiwa kufanyika kwa njia ya video siku ya Jumatatu jioni.

Blinken anaripotiwa kuihimiza China kuingia katika mazungumzo ya kutatua mvutano wake na Taiwan na kwa utaratibu unaoingiliana na matakwa ya raia wa kisiwa hicho.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents