Michezo

Martinez amtaka Lukaku kujiongezea thamani Man United

Kocha wa timu ya taifa ya Ubelgiji, Roberto Martinez amemtaka straika wa klabu ya Manchester United, Romelu Lukaku kuhakikisha anaongeza juhudi na kufanya vizuri ili kujiongezea thamani yake.

Kocha wa timu ya taifa ya Ubelgiji, Roberto Martinez

Martinez ambaye ni raia wa Hispania ameyasema hayo katika kipindi hiki ambacho Lukaku anakosolewa na mashabiki wa United kwa kushindwa kufunga mabao katika jumla ya michezo saba ya mashindano yote aliyocheza.

Straika wa klabu ya Manchester United, Romelu Lukaku

Romelu Lukaku anaechezea timu ya taifa ya Ubelgiji amesajiliwa na United kwa dau la paundi milioni 75 kipindi cha majira ya joto akitokea klabu ya Everton, kocha wa timu yake ya taifa Martinez amemtetea mchezaji huyo kwa kusema kuwa kushuka kwa kiwango chake ni kutokana na matatizo ya kisaikolojia.

“Nimenufaika na Romelu kwa kufanya nae kazi kwa zaidi ya miaka minne katika timu ya taifa ya Ubelgiji.” Amesema Martinez ambaye anakabiliwa na michezo dhidi ya Mexico na Japan.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents