Habari

Marufuku siasa za matusi na uchochezi Kinondoni – DC Ally Hapi

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi amewapiga marufuku Wanasiasa kutoa lugha za matusi na uchochezi kwenye wilaya yake huku akiwataka wachunge vinywa vyao wakati wanaongea .

Tokeo la picha la DC kinondoni ally hapi
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mh. Ally Hapi

DC Hapi amesema kila mwanasiasa anayetaka kufanya siasa kwenye wilaya yake ni lazima achunge mdomo wake kabla ya kuongea.

“Ni marufuku siasa za matusi na uchochezi katika wilaya ya Kinondoni.Kila anayetaka kufanya siasa Kinondoni na achunge kinywa chake,”ameandika DC Ali Hapi kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Jana DC ally Hapi alitoa tamko la kukamatwa kwa Mbunge wa jimbo la Kawe Mh. Halima Mdee kwa kile alichodai kuwa kwenye moja ya mikutano yake aliyoifanya kwenye wilaya yake alitoa kauli za kichochezi na kejeli kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh Dkt John Pombe Magufuli.

By Godfrey Mgallah

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents