Habari

Masanja Mkandamizaji atakiwa kujisalimisha ofisi ya mkuu wa wilaya baada ya kuwahoji wananchi kuhusu Corona – Audio

Masanja Mkandamizaji atakiwa kujisalimisha ofisi ya mkuu wa wilaya baada ya kuwahoji wananchi kuhusu Corona - Audio

Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Patrobas Katambi amemtaka Emmanuel Mgaya maarufu ‘Masanja Mkandamizaji’ kufika katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya au Polisi ili kohojiwa baada ya kuwahoji watu kiutani kuhusu #COVID19 akiwa Dodoma.


Amesema “Mmoja wa Watangazaji wa Vyombo vya Magharibi anaitwa Masanja amefanya utani kwenye maeneo ya Dodoma. Anataka kuthibitisha watu wa Dodoma hawaelewi kitu kuhusu Corona ila ametumia neno la Kiingereza la #COVID19“.

Ameeleza “Kwa mzaha huo tunataka kujua malengo yake nini hasa na kwanini amefanya hivyo Dodoma wakati hata DW nchini Ujerumani ugonjwa huo wameuchukulia ‘serious’ na kwanini hawajafanya popote ila Dodoma?”

Amesema kama hadi Jumatatu Masanja hajafika ama kwa Mkuu wa Mkoa au Mkuu wa Wilaya au Kituo cha Polisi basi akamatwe ili akaseme malengo yake ni yepi maana wao wako ‘serious’ kupambana na Corona.

Katika video fupi ya DW, Masanja ameonekana kuwauliza watu “Unafiriki hapa Dodoma mletewe COVID19 ngapi?” Na watu walikuwa wakijibu idadi kadhaa ya namba wanazotaka za COVID19.

By Ally Juma,.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents