Mara nyingi katika Jamii kumekuwako na kasumba mbalimbali kuhusu Suala zima la Masaji huku asilimia kubwa ya watu kwenye jamii huzani Masaji ni uhuni
Leo Mwana Dada Gloria Kasmili ambaye aliwahi kushiriki kwenye Mwanamke wa Shoka hatimaye amefunguka kwa kina juu ya Swala hili huku akitoa ufafanuzi mpana zaidi
Aidha Gloria Amefanikiwa kuongeza na kupanua biashara yake ambapo amezindua sehemu ya Masaji ya VVIP Maweni Kijaruba Kigamboni.
Ameongeza kuwa kwenye biashara yoyote ile lazima kuzingatia ubunifu na pia mteja anapofika sehemu anayotakiwa kupewa huduma anatakiwa kuhudumiwa bila kuwa na kero wala usumbufu wowote.