Burudani

Maunda Zorro ataja sababu za kutoa nyimbo chache na kwanini zinadumu kwa muda mrefu

Hadi sasa Maunda Zorro ana nyimbo nne tu za kwake mwenyewe. Miongoni mwa nyimbo hizo ni pamoja na ‘Niwe Wako’ na Mapenzi ya Wawili, lakini zimeendelea kuwa na maisha kila zinapochezwa.

Maunda Zorro akitumbuiza

Maunda ambaye ni dada yake na Banana Zorro na binti wa mwanamuziki mkongwe nchini, Zahir Ally Zorro amesema kwa kawaida hupenda kuachia nyimbo chache. “Sina haraka ya kutoa nyimbo kila mwaka, sio kwamba ndio inaprove kwamba wewe ndio mwanamuziki, natoa time inaruhusu kwamba sasa hivi I can, natoa. Saa zingine nakuwa nimebanwa na vitu vingine,” amesema.

Akiongelea siri ya kuandika nyimbo zenye maisha marefu, Maunda amesema ni kuandika nyimbo zenye hisia za ukweli.

“Kwangu mimi huwa naandika nyimbo ambayo ina ukweli sio fiction, sio kitu cha kufikirika. Naandika kitu ambacho kinagusa jamii hata kama sio cha kwangu, kimetokea sehemu fulani, kimemtokea mtu fulani. Kwa mfano kama nilivyoandika ‘Niwe Wako’, watu wanapendana kila siku. Ndio maana hata ukisiliza hata mwakani bado utahisi kama ni nyimbo mpya na bado inakugusa kwa njia moja ama nyingine.”

Maunda amesema anatarajia kuachia wimbo wake mpya mwishoni mwa mwezi huu na amesema utakuwa na mahadhi ya taratibu. “Sasa hivi I am thinking of slow tena, nahisi I am way good kwenye slow, kwahiyo sasa hivi nategemea kutoa slow.”

Msikilize zaidi hapa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents