Burudani

Izzo Bizness azungumzia kijacho baada ya ‘Tummoghele’ (Audio)

Rapper kutoka Mbeya City, Emmanuel Simwinga aka Izzo Bizness amesema hakutegemea wimbo wake wa sasa ‘Tummoghele’ ungekuwa na mafanikio makubwa kama anayoyaona sasa.

izzo

Amesema katika muda miezi michache tangu wimbo huo na video yake vitoke, ameshangaa kuona watu wanauimba mwanzo mwisho anapokuwa akiutumbuiza jukwaani kitu ambacho kimempa moyo. “Imenitia nguvu sana na nimeona kweli muziki unafika na kuna namna ya kuufikisha sehemu. Nimefanikiwa kwa kiasi kikubwa sababu hakuna muda ambao msanii anajisikia raha kama unapofika sehemu watu wanaimba mashairi ya nyimbo, unaweza ukakaa kimya watu wakaimba chorus,” amesema.

Ameongeza kuwa wakati anatoa wimbo huo, kuna watu walimkatisha tamaa kutokana na jina lake lakini imekuja kuwa tofauti na kwamba wimbo wake unaokuja utakuwa na surprise pia na ni muziki ambao wengi wanahisi ameacha kuufanya.

Msikilize zaidi hapa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents