Mahojiano

Mayunga aeleza ndoto zake za kufanya collabo na Chris Brown baada ya Akon “Tanzania natamani kufanya na Diamond Alikiba na Mwana FA” – Video

Mayunga aeleza ndoto zake za kufanya collabo na Chris Brown baada ya Akon "Tanzania natamani kufanya na Diamond Alikiba na Mwana FA" - Video

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva @mayungaa aliyewahi kuwa mshindi wa shindano la Airtel Trace music Star ambaye alipata nafasi ya kufanya Collabo na @akon aeleza kilichomkwamisha Kimataifa.


Mbali na hilo @mayungaa amefunguka na kueleza ndoto zake za kufanya kazi na mkali kutoka Marekani @chrisbrownofficial Kwa Tanzania Mayunga amewataja wengi sana wakiwemo @harmonize_tz @officialalikiba @diamondplatnumz @mwanafa na hasa wasanii wa R&B kama @iambenpol na @belle9tz

Pia ameongelea suala la ushirikiano Kwa wasanii pia upendo kitu ambacho kwa wasanii wa Tanzania inakuwa ngumu sana. Mayunga ametutonya pia kinachowapa ugumu wasanii wa Kitanzania kufanya Show kubwa Marekani kama wasanii wa Nigeria akisema wengi hufanya show wakiwa Watanzania na Wakenya kidogo kitu ambacho bado wasanii wa Kitanzania wana kazi kubwa ya kufanya ili kuteka kila aina ya mtu anayeishi Marekani ukiachilia watu kutoka Afrika Mashariki.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents