Burudani

‘Mazishi’ ya Khaligraph ilinivutia kufanya naye collabo

Christian Bella amesema wimbo Mazishi wa Kaligraph ndio ulimvutia kumshirikisha kwenye wimbo wake mpya, Ollah.

Akizungumza na Eddy Msafi kupitia kipindi cha Full Charge cha Pride FM ya Mtwara, Bella amedai kuwa baada ya kufanya wimbo huo yeye na timu yake walishauriana kutafuta rapper, wa nje ya Tanzania kushirikishwa kwenye wimbo huo.

Ameongeza kuwa katika kuchekecha akili, Khaligraph alipendekezwa zaidi na akaamua kumtafuta.

Ameeleza kuwa kuwa alimtafuta rapper huyo kupitia DM ya Instagram na Khaligraph alifurahia ofa hiyo kwakuwa naye ni shabiki mkubwa wa ngoma za Bella.

Baada ya makubaliano hayo alimtumia beat na chorus rapper huyo ili kuandika verse zake na mwishowe kumfuata Nairobi ili kuingiza sauti zake na kumalizia video iliyoongozwa na Hanscana.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents